AfDB yaidhinisha dola za kimarekani milioni 5.4 ili kuimarisha usalama wa chakula nchini Somalia
2022-07-22 08:36:14| CRI

Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imeidhinisha kiasi cha dola za kimarekani milioni 5.4 kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Afrika, ili kuchangia usalama wa chakula unaohitajika nchini Somalia.

Mkurugenzi mkuu wa Benki hiyo kanda ya Afrika Mashariki, Nnenna Nwabufo, amesema kwenye taarifa iliyotolewa Jumatano kuwa, athari za ukame wa muda mrefu na athari za mgogoro kati ya Russia na Ukraine zimeongeza uhaba wa chakula nchini humo. 

Nwabufo ameongeza kuwa, fedha hizo ni ufadhili wa ziada kwa Mpango wa Kimataifa wa Kujenga Ufufuaji wa Usalama wa Chakula na Lishe, na utasambaza mbegu bora zilizoidhinishwa kuendana na hali ya hewa na kuwezesha uzinduzi wa benki za malisho katika mikoa sita nchini humo.