Tanzania yazindua hekta zaidi ya elfu 11 kwa ajili ya kilimo kwa vijana
2022-07-25 08:48:10| CRI

Mamlaka nchini Tanzania zimezindua eneo la mashamba la hekta 11,453 kwa ajili ya vijana mkoani Dodoma.

Waziri wa Kilimo nchini humo, Hussein Bashe amesema hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa taifa wa kilimo kwa ajili ya vijana. Amesema mashamba hayo yako katika vijiji vya Mlazo na Ndogoe katika wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, na kwamba kilimo hicho kitaenda sambamba na uchimbaji wa mabwawa kwa ajili ya umwagiliaji, ambao utasimamiwa na Kamati ya Taifa ya Umwagiliaji kwa uratibu na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka ya Dodoma Mjini (DUWASA).

Ameongeza kuwa, tayari wataalamu wamepima udongo katika maeneo ya mashamba yaliyotengwa kwa ajili ya vijana ili kutambua aina ya mazao yanayofaa kulimwa katika mashamba hayo.