China kushiriki kama “nchi ya heshima”kwenye maonesho ya biashara na kilimo ya Zambia
2022-07-26 08:25:04| CRI

China itashiriki kama “nchi ya heshima” kwenye maonesho ya 94 ya Biashara na Kilimo ya Zambia yatakayoanza wiki hii.

Maonesho hayo ambayo yanarejea baada ya kusitishwa kwa miaka miwili kutokana na janga la COVID-19, yatafanyika kuanzia Julai 27 hadi Agosti 1, chini ya kaulimbiu  ya “Uvumbuzi kupitia Teknolojia, Teknolojia Yabadili Biashara”.

Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Ushirika vya Kilimo na Biashara nchini Zambia Duncan Mfula, amesema, uamuzi wa kuialika China kama “nchi ya heshima” umetokana na serikali ya China kuzihamasisha kampuni 110 za nchi hiyo kushiriki kwenye maonesho hayo.

Bw. Mfula amesema, kati ya nchi zaidi ya 20 za kigeni zitakazoshiriki kwenye maonesho hayo, China ni nchi pekee inayopeleka idadi kubwa ya kampuni kwenye maonyesho hayo.