Bunge la Somalia lamwongezea siku 10 Waziri Mkuu kuunda Baraza la Mawaziri
2022-07-26 08:22:45| CRI

Bunge la Somalia limeridhia kumwongezea waziri mkuu wa nchi hiyo Hamza Abdi Barre siku 10 zaidi kuunda serikali yake.

Barre alitarajiwa kutangaza Baraza lake la Mawaziri jana jumatatu, ikiwa ni siku 30 baada ya kuteuliwa, lakini amesema bado hajamaliza majadiliano kuhusu uundwaji wa Baraza hilo, na kulitaka Bunge kumwongezea muda ili aunde serikali jumuishi.

Amesema Somalia iko njia panda na inatakiwa kusonga mbele, hivyo anapaswa kuunda uongozi utakaotekeleza mabadiliko na maendeleo ambayo watu wa Somalia wanayahitaji.

Alipokutana na mashirika ya kiraia, Barre alieleza nafasi ya vijana wa Somalia katika kushiriki kwenye maendeleo, akisema vijana ndio hatma ya baadaye ya nchi hiyo na ushauri wao ni muhimu katika kuunga mkono serikali.