Kikosi cha 25 cha walinda amani wa China nchini DRC chatunukiwa nishani ya amani ya UM
2022-07-26 08:25:49| CRI

Wanajeshi wote 218 wa kikosi cha 25 cha walinda amani wa China nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) jana Jumatatu walitunukiwa nishani ya amani ya Umoja wa Mataifa kwenye kambi yao mkoani Kivu Kusini.

Kamanda wa kikosi hicho Bw. Deng Liang amesema, wanajeshi wote wa kikosi chake wanathamini heshima hiyo, na kuendelea kutekeleza vizuri majukumu waliyopewa, ili kutoa mchango mkubwa zaidi kwa ajili ya amani na maendeleo ya dunia.