Kenya yazindua kituo kipya cha kuzalisha umeme kutoka joto la ardhini ili kuongeza upatikanaji wa nishati safi
2022-07-27 08:57:15| CRI

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amezindua kituo kipya cha kuzalisha umeme kwa kutumia joto kutoka ardhini, ambalo litaongeza megawati 83.3 zaidi katika gridi ya taifa na kuendeleza upatikanaji wa nishati safi nchini humo.

Rais Kenyatta amesema, kituo hicho kinachoitwa Olkaria 1 kinachomilikiwa na kuendeshwa na Kampuni ya Uzalishaji Umeme ya Kenya (KenGen) kinaendana na mpango wa kupunguza gharama za nishati ili kuunga mkono mpango wa maendeleo wa taifa hilo.

Amesema serikali yake imeweka mipango imara ili kuhakikisha kuwa nchi hiyo inatimiza asilimia 100 ya matumizi ya nishati safi itakapofika mwaka 2030.