Watu 19 wauawa na wengine 23 wajeruhiwa katika mashambulizi ya mabomu Somalia
2022-07-28 09:05:07| CRI

Watu 19 wameuawa na wengine 23 kujeruhiwa katika mashambulizi tofauti ya mabomu yaliyotokea jana Jumatano katika miji miwili kusini mwa Somalia.

Katika shambulizi la kwanza lililotokea katika mji wa Marka katika jimbo la Lower Shabelle, mshambuliaji wa kujitoa mhanga alijilipua nje ya ofisi ya usimamizi wa mji huo na kusababisha vifo vya watu 13 akiwemo mkuu wa wilaya Abdullahi Ali Wafow na watu wengine watano kujeruhiwa. Kundi la al-Shabab limetangaza kuhusika na shambulizi hilo.

Katika shambulizi la pili, watu sita waliuawa na wengine 18 kujeruhiwa katika milipuko miwili ya mabomu yaliyotegwa kando ya barabara katika mji wa Afgoye jimbo la Lower Shabelle.