China na Afrika zasaini makubaliano ya miradi ya uchumi na biashara yenye thamani ya dola milioni 170 za kimarekani
2022-07-29 09:09:46| CRI

China na baadhi ya nchi za Afrika zimesaini jumla ya miradi na makubaliano 14 ya ushirikiano wa kibiashara na kiuchumi yenye thamani ya dola milioni 170 za kimarekani mkoani Hunan, katikati ya China.

Makubaliano hayo yanayohusisha sekta mbalimbali ikiwemo ushirikiano wa kikanda, makubaliano ya kimkakati, ufadhili wa mradi, ushirikiano wa uwekezaji na maagizo ya kibiashara, yamesainiwa katika kikao cha kutangaza ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Afrika kilichofanyika Changsha, mji mkuu wa mkoa wa Hunan.

Katika kikao hicho, idara za kibiashara za mikoa sita pia zimesaini kwa pamoja makubaliano ya kuhimiza ushirikiano wa kiuchumi na mawasiliano ya kibiashara na nchi za Afrika.

Mabalozi 29 kutoka nchi 15 za Afrika ikiwa ni pamoja na Algeria, Ethiopia, Angola, Ghana na Kenya walihudhuria kikao hicho, ambacho pia kimetangaza kuanzishwa kwa Eneo la Majaribio la Ushirikiano wa Kina wa Uchumi na Biashara kati ya China na Afrika.