Kenya yatoa dozi milioni 20 za chanjo ya COVID-19
2022-07-29 08:53:56| CRI

Wizara ya Afya nchini Kenya imesema imetoa dozi zaidi ya milioni 20 za chanjo ya COVID-19, ikiwa ni hatua kubwa katika kupambana na janga hilo.

Waziri wa Wizara hiyo Mutahi Kagwe amesema katika taarifa yake iliyotolewa jijini Nairobi kuwa, kati ya dozi hizo milioni 20, milioni 17 zimetolewa kwa watu wazima na zilizobaki kwa vijana wenye umri wa miaka kati ya 15 mpaka 18.

Julai 13, Kenya ilitangaza kuwa imetoa chanjo ya COVID-19 kwa watu milioni 19, ikiashiria kuwa nchi hiyo imetoa karibu dozi milioni moja katika wiki mbili.

Mpaka kufikia jana Alhamis, idadi ya kesi zilizothibitishwa kuwa na COVID-19 ilikuwa ni 337,500.

Kenya imepokea dozi milioni 27.8 za chanjo za COVID-19, ikijumuisha chanjo za Sinopharm kutoka nchini China.