OCHA: watu elfu 31 wapoteza makazi yao kutokana na mapambano katika jimbo la Blue Nile, Sudan
2022-08-02 09:35:53| CRI

Ofisi ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) imesema mapambano kati ya jamii katika jimbo la Blue Nile nchini Sudan yamesababisha watu 31,000 kupoteza makazi yao.

Ikinukuu ripoti za awali kutoka serikali za mitaa na washirika, OCHA imesema mwezi uliopita, watu wapya walipoteza makazi yao mjini Ganis jimboni humo.

Ofisi hiyo imesema hali ya sasa ya mji wa Ed Damazine na sehemu nyingine za jimbo la Blue Nile ni ya utulivu, lakini haiwezi kukadiriwa . Kuanzia mwezi Januari hadi Juni mwaka huu, mapambano yamesababisha watu zaidi ya 117,000 kupoteza makazi yao huko Sudan.

OCHA imesema wadau wa masuala ya kibinadamu wanawapatia msaada wakimbizi na wengine walioathiriwa, kwa kutoa msaada wa miezi mitatu kwa watu elfu 30.