Wahamiaji haramu zaidi 2900 wakamatwa kaskazini magharibi mwa Tanzania katika miezi 6
2022-08-03 09:29:17| CRI

Idara ya uhamiaji ya Tanzania jana ilisema, wahamiaji haramu wasiopungua 2940 wamekamatwa katika mkoa wa Kagera, kaskazini magharibi mwa nchi hiyo kati ya mwezi Januari na Juni mwaka huu.

Kiongozi wa Idara ya Uhamiaji ya Tanzania mkoani Kagera Thomas Fussy amesema, wahamiaji haramu hao wamekamatwa kwenye operesheni maalumu katika miezi sita.

Ameongeza kuwa, wahamiaji hao walitoka nchi tofauti zikiwemo Rwanda, Kenya, DRC, Zimbabwe, Ethiopia, Somalia, Burundi, Uganda na Zambia.