Kenya yaimarisha usalama katika eneo la kaskazini magharibi kutokana na wasiwasi wa kiusalama kufuatia uchaguzi
2022-08-03 09:26:05| CRI

Waziri wa usalama wa ndani wa Kenya Bw. Fred Matiang'i jana alisema Kenya imeimarisha usalama kwenye baadhi ya maeneo ya kaskazini magharibi mwa nchi hiyo baada ya kusambazwa kwa vipeperushi vinavyoeneza chuki kabla ya uchaguzi mkuu utakaofanyika wiki ijayo.

Amesema watuhumiwa wanane wamekamatwa kutokana na kusambaza vipeperushi hivyo kwenye baadhi ya maeneo ya mkoa wa bonde la ufa. Polisi wanakusanya habari nyingi zaidi, na kazi ya uchunguzi bado inaendelea kufanyika, ambapo watawatafuta hadi wapangaji wa tukio hilo, ambao wanawaonya watu wa jamii husika kwamba wataadhibiwa kama hawatawapigia kura viongozi mahususi.