Mwenyekiti wa Kikundi cha Urafiki kati ya Kenya na China cha bunge la Kenya alaani ziara ya Pelosi Taiwan
2022-08-04 11:08:29| CRI

Mwenyekiti wa Kikundi cha Urafiki kati ya Kenya na China cha Bunge la Kenya Shakeel Shabbir ametoa taarifa, akipinga na kulaani ziara ya Spika wa Baraza la Wawakilishi la Bunge la Marekani Nancy Pelosi huko Taiwan nchini China.

Shabbir amesema, Kenya inafuata kanuni ya kuwepo kwa China moja duniani, na kuunga mkono kithabiti msimamo wa China katika suala la Taiwan, na kuunga mkono juhudi zake za kutimiza umoja wa kitaifa, pamoja na hatua zake za kulinda mamlaka, ukamilifu wa ardhi, na amani na utulivu wa sehemu ya Taiwan.