Afrika inaweza kujifunza nini kutokana na uzoefu wa China?
2022-08-04 09:13:36| cri


Na Umaru Napoleon Koroma,

Katibu mkuu wa Chama cha Umma cha Sierra Leone


Kwenye hotuba iliyotolewa na Makhtar Diop, Naibu Mkuu wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika, alisema mwaka 1978 China ilikuwa miongoni mwa nchi maskini zaidi duniani. Kuanzia mwaka huo, mapato halisi ya kila mtu wa China yameongezeka, kwa wastani wa zaidi ya asilimia 8 kwa mwaka,  hiki ni kiwango cha kushangaza cha ukuaji wa uchumi.

Mwaka 2010 China ikawa nchi ya pili kwa nguvu za kiuchumi duniani nyuma ya Marekani, na kuipiku Japan kwa msingi wa Pato la Taifa linalohesabiwa kwa dola zaMarekani. China imekuwa nchi yenye viwango kama nchi yenye nguvu ya viwanda, muuzaji mkubwa zaidi wa bidhaa kwa nchi za nje na mmiliki wa akiba kubwa ya fedha za kigeni. Wakati huo huo zaidi ya watu milioni 800 wameondolewa kutoka kwenye umaskini uliokithiri katika muongo mmoja tu wa maendeleo ya kiuchumi, na wastani wa maisha ya watu wa China umeongezeka kwa kiasi kikubwa kutoka miaka 35 hadi miaka 77.

Katika kipindi hicho wakati China inatekeleza dhana yake ya ukuaji wa uchumi, Afrika pia imejitahidi kupata viwango vya ukuaji wa uchumi, ingawa viko tofauti katika nchi zote na viwango vyake vinatofautiana kulingana na kanda. Viwango kutokuwa na uwiano na kutofautiana kunaifanya hali ya uchumi wa Afrika isitabirike na lakini pia haiwezi kufanywa kuwa ni hali ya jumla, kwani kuna nchi tajiri kwa maliasili zinazokua kwa kasi zaidi kuliko zile zisizo na maliasini.


Ni nini ambacho Afrika inaweza kujifunza kutoka kwa China?

1. Uongozi imara. Ikiwa ni nchi yenye idadi ya watu bilioni 1.4, miujiza ya mafanikio ya China isingewezekana bila uongozi imara. Kwa kuzingatia historia ya nchi hiyo kubwa, ni dhahiri kwamba mababu wa China walijaribu na kutafiti mifumo mbalimbali ya kisiasa kwa ajili ya watu wao. Mifumo mingi haikuonekana kufanya kazi kwa sababu ya tofauti za miundo ya kitamaduni na kijamii ya watu wake kote nchini. Kwenye orodha ya mifumo ya kisiasa kulikuwa na mifumo kama vile utawala wa kifalme wa kikatiba, mfumo wa bunge na mfumo wa urais n.k. lakini hakuna mfumo hata mmoja kati ya huo ulioweza kuiepusha China na machungu.

Hata hivyo, baada ya changamoto zote za mifumo ya kisiasa, Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kilionyesha uwezekano mkubwa wa kuleta utulivu kilianzishwa mwaka 1921. CPC kiliendelea kuwaongoza watu katika kutafuta njia ya kimapinduzi na ya maendeleo inayoendana na hali ya China na kuleta mfumo wa kisiasa wenye sifa wa kipekee wa China. Chini ya uongozi wa CPC, China bila shaka imedumisha ukuaji endelevu wa uchumi na utulivu wa kijamii.

2. Mfumo wa kipekee wa kidemokrasia wa China. CPC kinatekeleza kwa uwazi demokarasia  ya umma inayohusisha maeneo yote ya mchakato wa kidemokrasia kwa sekta zote za jamii. Mchakato huo unajumuisha mfumo wa mabaraza ya umma, mfumo wa ushirikiano wa vyama vingi na mashauriano ya kisiasa pamoja na mfumo wa makabila kujiendesha wa kikanda na ngazi ya Jumuiya kujiendesha. Jukwaa hili la kisiasa lenye tofauti lakini jumuishi, kuna zaidi ya wajumbe  milioni 2.6 katika mabunge ya umma katika ngazi zote nchini China, ambapo takriban 95% wanachaguliwa moja kwa moja. Takriban wajumbe 3,000 wa Bunge la Umma la China (NPC) wanachaguliwa kwa njia isiyo ya moja kwa moja na wajumbe  wa mabunge ya ngazi ya mikoa, na wajumbe  hao huchagua viongozi wa serikali. Mfumo huu wa kipekee umeziwezesha sera za Chama na serikali kutekelezwa na kufikia malengo ya maendeleo.

3. Sababu ya uhuru na kujitegemea. Moyo wa kipekee wa Wachina wa uhuru na kujitegemea umedumishwa katika historia ya nchi hiyo haswa katika siku za hivi karibuni. Rais Xi Jinping wa China alisema "Historia nzima ya China tangu zama za sasa inatuambia kwamba mambo nchini China lazima yafanywe kwa kuzingatia hali ya China na uhalisia wa China, ambayo ni njia sahihi ya kutatua matatizo yote ya China." Katika miaka ya 1960 na 1970, Marekani ilizizingira China na Umoja wa Kisovieti, ikakata misaada kwa China, na katika mazingira magumu sana wanasayansi wa China wakitegemea kabisa majaribio yao wenyewe walifanikiwa kutengeneza satelaiti ya kwanza ya China mwaka 1970. Marekani na Ulaya zilipokataa kushirikiana na China, China ilianzisha mpango wake wa kituo cha anga za juu na sasa inaendesha kituo hicho kwa kujitegemea na kuishangaza dunia nzima.

4. China kuikumbatia dunia. China ilijifunza somo gumu kutokana na   hali yake ya kujifungia mlango na kuanza kufanya mageuzi na sera ya kufungua  mlango mwishoni mwa miaka ya 1970. Sera hii imeongeza sana uzalishaji wa China na kuifanya China kuwa "kiwanda cha dunia". Sasa China imejiweka wazi kwa dunia na zaidi ya hapo imetoa pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" (BRI) kwa lengo la kuhimiza muunganiko wa mabara ya Asia, Ulaya na Afrika na bahari zao zinazopakana. Sera hii imeanzisha na kuimarisha ushirikiano kati ya nchi zinazoshiriki kwenye pendekezo hilo; kuanzisha mitandao ya maunganisho ya pande zote, ngazi tofauti na yenye mchanganyiko, na kutambua maendeleo mseto, huru, yenye uwiano na endelevu katika nchi mbalimbali. Kutokana na kuungwa mkono na nchi 145 na mashirika 32 ya kimataifa, pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja"  linakua  haraka na kuwa “ukanda wa maendeleo” unaonufaisha dunia nzima na kuwa “njia ya furaha” kwa watu wote.


Kwa kumalizia, uzoefu wa China ni zaidi ya hayo yaliyowasilishwa hapo juu, lakini mambo manne yaliyowasilishwa hapo ni miongoni mwa mambo muhimu zaidi ambayo Afrika inaweza kujifunza kutoka kwa China. Mfumo wa China unatoa fursa za ukuaji. Nchi za Afrika zinapaswa kutarajia kujumuisha kanuni muhimu za ukuaji wa kuvutia wa China kwenye mikakati ya mipango ya maendeleo yao wanapojaribu kujenga uchumi katika miaka ya hivi karibuni. Katika siku za baadaye tunatumai kuwa Afrika inaweza kuitazamia China sio tu kama mshirika wake wa kibiashara, lakini pia kama mwalimu wa ukuaji wa uchumi.