Umoja wa Mataifa waonya juu ya uwezekano wa uhaba wa chakula nchini Sudan
2022-08-04 11:12:13| CRI


 

Ofisi ya Uratibu na Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) imesema kuwa Umoja wa Mataifa umerejea tena maonyo yake juu ya uwezekano wa kutokea uhaba wa chakula nchini Sudan, kutokana na kuendelea kukosekana kwa ufadhili wa kimataifa.

Hali ya kibinadamu nchini Sudan iliendelea kutia wasiwasi sana, kwa kuongezeka kwa kasi kwa uhaba wa chakula, raia wengi zaidi kukimbia makazi yao na kuwasili kwa wakimbizi wengi zaidi kutoka nchi jirani, wengi wao kutoka Sudan Kusini, Ethiopia na Eritrea.

Wakati huo huo, Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) nchini Sudan limetangaza kuwa limelazimika kupunguza mgao wa wakimbizi kote nchini kuanzia mwezi Juni kwa sababu ya uhaba mkubwa wa fedha.