AU na COMESA zaanzisha ujumbe wa pamoja wa waangalizi wa uchaguzi wa Kenya
2022-08-05 09:05:43| CRI

Umoja wa Afrika (AU) na Soko la Pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA) jana walianzisha ujumbe wa pamoja wa waangalizi wa uchaguzi wa Kenya, utakaofanyika tarehe 9 mwezi Agosti.

Kiongozi wa ujumbe huo ambaye ni rais wa zamani wa Sierra Leone Ernest Bai Koroma amesema ujumbe wake wenye waangalizi 90 unaundwa na serikali, nchi wanachama, bunge la AU, mashirika ya kijamii na vyombo vinavyosimamia uchaguzi barani Afrika. Ujumbe huo utajitahidi kuhimiza uchaguzi wa amani, huru, usawa, uwazi na uaminifu, kitendo ambacho kitaimarisha mchakato wa kidemokrasia nchini Kenya.

Habari kutoka ujumbe huo imesema timu ya muda mfupi ya waangalizi itapelekwa kwenye maeneo mbalimbali ya uchaguzi nchini Kenya siku ya Jumapili. Koroma ameongeza kuwa kazi ya ujumbe wake ni kutoa tathmini huru na isiyo na upendeleo, juu ya mchakato wa uchaguzi wa Kenya kama ilivyoelezwa kwenye kanuni na vigezo vya kimataifa.