Vikosi vya usalama vya Ethiopia vyawaua washukiwa 333 wa uasi
2022-08-08 08:43:40| cri

Waziri wa Huduma ya Mawasiliano ya Serikali ya Ethiopia Selamawit Kassa amesema, vikosi vya usalama vya nchi hiyo vimewaua watu 333 wanaoshukiwa kuwa waasi wa Jeshi la Ukombozi wa Oromo (OLA) na kuwakamata washukiwa wengine 671 katika operesheni ya hivi karibuni ya usalama.

Kassa pia amesema idadi kubwa ya silaha na mifumo ya mawasiliano ya redio ilikamatwa wakati wa operesheni hiyo iliyoanza tarehe 23 hadi tarehe 29, mwezi uliopita.