EAC yapeleka waangalizi wa uchaguzi nchini Kenya kabla ya uchaguzi mkuu
2022-08-08 08:56:41| CRI

Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imepeleka timu 15 za waangalizi  wa  uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika kesho jumanne nchini Kenya.

Taarifa iliyotolewa na Jumuiya hiyo imesema, mkuu wa Tume ya waangalizi wa Uchaguzi ya EAC, ambaye ni rais wa zamani wa Tanzania Jakaya Kikwete, amesema waangalizi hao wamepata mafunzo ya kina ya siku tano yatakayowawezesha kutimiza wajibu wao kama wasimamizi wa kimataifa na pia kama wasimamizi wa EAC.

Amesema jukumu kuu la waangalizi hao ni kufuatilia kampeni za uchaguzi zinazoendelea, kufuatilia mchakato wa upigaji kura, ikiwemo usimamizi wa matokeo katika vituo vya kupigia kura, kufuatilia hesabu ya kura, matangazo, na kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi huo.