Umoja wa Afrika walaani mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Isarel dhidi ya Gaza
2022-08-09 08:34:39| cri

Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika Bw. Moussa Faki Mahamat Jumapili alilaani mashamulizi ya anga yaliyofanywa na Isarel dhidi ya Gaza.

Bw. Mahamat amesema, kitendo cha vikosi vya usalama vya Israel kulenga raia wa kawaida na kuchukua ardhi ya Palestina kimekiuka sheria ya kimataifa, pia kimeongeza utatanishi katika kutafuta suluhisho la haki na la kudumu kati ya pande hizo.

Bw. Mahamat amesisitiza kuwa, Umoja wa Afrika unaunga mkono matakwa ya Wapalestina ya nchi huru yenye mamlaka ambayo Jerusalem Mashariki ni mji mkuu wake.