Sudan yalaani aina zote za itikadi kali na ugaidi
2022-08-09 08:35:00| CRI

Mwenyekiti wa Baraza la Utawala wa Mpito la Sudan Abdel Fattah Al-Burhan amesisitiza msimamo wa nchi hiyo wa kulaani aina zote za siasa kali, ugaidi na uhalifu.

Al-Burhan aliyasema hayo alipotoa hotuba katika semina iliyoandaliwa na Kamati ya Huduma za Ujasusi na Usalama wa Afrika (CISSA) katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum, kuhusu “jukumu la kuondoa siasa  kali na ufufuaji wake katika kupambana na ugaidi”. Amesema kama nchi nyingine, Sudan inakabiliwa na changamoto za siasa  kali na ugaidi, na inafanya jitihada kubwa za kupambana na changamoto hizo kwa njia mbalimbali, ikiwa ni pamoja na idara za usalama, utungaji wa sheria, na kujiunga na makubaliano ya kikanda, kimataifa na kati ya nchi.

Al-Burhan amesisitiza jukumu la CISSA katika kukabiliana na ugaidi,  siasa kali, uhalifu wa kuvuka mipaka na uhamiaji haramu pamoja na kukabiliana na changamoto zote za usalama katika Bara la Afrika.