Ukame mkali waathiri Wasomalia zaidi ya milioni 1
2022-08-10 08:40:10| cri

Ofisi ya Umoja wa Mataifa Inayoratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imesema, watu 1,002,796 wamekimbia makazi yao kutokana na ukame nchini Somalia tangu Januari 2021.

Mwezi uliopita, Shirika hilo liliomba msaada wa dola za kimarekani milioni 993.3 ili kutoa msaada wa kuokoa maisha na kuzuia njaa na kukabiliana na ukame nchini Somalia kabla ya mwezi Desemba.

Shirika hilo limesema, athari za ukame na kuongezeka kwa shinikizo la kiuchumi vinazidisha mahitaji hayo na kuifanya nchi hiyo kuwa hatarini kukumbwa na baa la njaa.