China yatoa waraka kuhusu suala la Taiwan, na muungano wa taifa katika zama mpya
2022-08-10 14:45:46| cri

Ofisi inayoshughulikia mambo ya Taiwan ya baraza la serikali la China na ofisi ya habari ya baraza la serikali la China, wametoa waraka kuhusu “suala la Taiwan na muungano wa China katika zama mpya”.

Waraka huo umesisitiza ukweli kuhusu Taiwan kuwa sehemu ya China, na kuonesha nia thabiti ya Chama cha Kikomunisti cha China, watu wa China na nia yao ya kuunganisha taifa, na kusisitiza msimamo na sera za Chama cha Kikomunisti cha China na serikali ya China katika zama mpya.

Waraka huo unasema Taiwan ni sehemu ya China tangu zama za kale, na kauli hii ina msingi wa kihistoria na kisheria.

Waraka pia unasema azimio nambari 2758 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ni waraka wa kisiasa ambao ni msingi wa sera ya China moja, ambao mamlaka yake kisheria hayana shaka na yanatambuliwa na dunia nzima.

Waraka umesisitiza kuwa kuna China moja, na Taiwan ni sehemu ya China. Ukweli huu haupingiki na unaungwa mkono na historia na sheria. Taiwan haijawahi kuwa nchi, na hadhi yake ya kuwa sehemu ya China haina mbadala.