Askari 15 wauawa katika mlipuko nchini Burkina Faso
2022-08-10 08:39:21| CRI

Askari 15 wameuawa katika shambulizi la kigaidi lililotokea jana dhidi ya msafara uliowasindikiza wanajeshi katika barabara  ya kutoka Bourzanga kwenda Djibo, nchini Burkina Faso.

Taarifa iliyotolewa na jeshi la nchi hiyo imesema, moja ya magari katika msafara huo lililokuwa limebeba wanajeshi lilikanyaga bomu lililotengenezwa kienyeji karibu na wilaya ya Namsiguia, mkoa wa Bam, na kuongeza kuwa, bomu la pili lililipuliwa kutoka mbali, na kusababisha vifo na majeruhi, na kwamba kazi ya uokoaji na operesheni za usalama zinaendelea.

Hali ya usalama nchini Burkina Faso imekuwa mbaya zaidi tangu mwaka 2015 kufuatia mashambulizi yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 1000 na wengine zaidi ya milioni 1.9 kukimbia makazi yao.