UM na Ethiopia zatoa wito wa uchangishaji wa dola za kimarekani milioni 73 kusaidia wakimbizi
2022-08-10 08:40:17| CRI

Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP), Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) na Huduma ya Kuhudumia Wakimbizi ya Serikali ya Ethiopia kwa pamoja zimetoa wito wa kuchangisha  dola za kimarekani milioni 73 ili kutoa mgawo wa chakula kwa zaidi ya wakimbizi 750,000 wanaoishi nchini humo.

Katika taarifa yao ya pamoja kwa vyombo vya habari, mashirika hayo yamesema fedha hizo ni muhimu ili kukabiliana na mgawo wa chakula unaohitajika kwa wakimbizi katika miezi sita ijayo.

Uhaba wa chakula kati ya wakimbizi wanaoishi nchini Ethiopia umeongezeka kutokana na kupunguzwa kwa kiasi cha chakula kinachotolewa, na hali imezidi kuwa mbaya kutokana na uhaba wa chakula duniani, mapigano, kuongezeka kwa bei za vyakula na nishati, na pia kutokana na athari za janga la COVID-19.