China yasema maoni ya Waafrika kuhusu ushirikiano kati ya China na Afrika ni muhimu
2022-08-10 08:39:46| cri

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Wang Wenbin jana alisema, maoni ya Waafrika kuhusu suala la ushirikiano kati ya China na Afrika ni ya muhimu zaidi kuliko maoni ya Marekani.

Wang amesema hayo kufuatia Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Anthony Blinken kufanya ziara nchini Afrika Kusini tarehe 8 mwezi huu, ambapo alisema, Marekani haitaki kuzilazimisha pande mbalimbali kuchagua  upande wa Marekani au upande wa China. .

Wang amesema, China inaishauri Marekani kusikiliza na kuheshimu matakwa ya nchi za Afrika na wananchi wao, na kama Marekani inataka kuisaidia Afrika kwa moyo wa dhati, inapaswa kuchukua vitendo  halisi, na wala si kuufanya mkakati kwa Afrika kuwa chombo cha kuzuia na kushambulia ushirikiano kati ya nchi nyingine na Afrika.