Sierra Leone yatangaza amri ya kutotoka nje kufuatia maandamano makubwa
2022-08-11 08:29:29| cri

Makamu wa Rais wa Sierra Leone Mohamed Juldeh Jalloh jana ametangaza amri ya kutotoka nje kufuatia maandamano makubwa nchini humo, ikiwa ni hatua ya kutuliza hali na kurejesha nchi hiyo katika hali ya kawaida.

Jana jumatano, maelfu ya waandamanaji waliingia katika mitaa ya mji mkuu wa nchi hiyo Freetown na baadhi ya maeneo mengine ya nchi, wakiitaka serikali kukabiliana na suala la hali ngumu ya kiuchumi na gharama ya juu ya maisha.

Serikali imelitaka jeshi la nchi hiyo kushirikiana na polisi ili kukabiliana na maandamano hayo.