Zaidi ya malori 4000 yapeleka misaada ya kibinadamu mkoani Tigray nchini Ethiopia
2022-08-11 08:32:20| CRI

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) limesema, jumla ya malori 4,765 yaliyobeba vifaa vya misaada yameingia mkoani Tigray, Ethiopia, tangu mwezi April mwaka huu.

Katika ripoti yake ya hivi karibuni kuhusu hali ya dharura nchini Ethiopia iliyotolewa jana jumatano, Shirika hilo limeonya kuwa, uhaba wa mafuta bado ni kizuizi kikubwa katika kudumisha operesheni za misaada mkoani Tigray, na kuzuia mwendelezo wa usambazaji wa vifaa vya misaada kutoka Mekelle, mji mkuu wa mkoa huo kwenda katika maeneo mengine.

Shirika hilo limesema, hali ya kibinadamu nchini Ethiopia inaendelea kuwa na athari mbaya kwa wakimbizi pamoja na wakimbizi wa ndani na jamii zilizowapokea wakimbizi hao.