UM yaipongeza Sudan Kusini kwa kuongeza muda wa serikali ya mpito
2022-08-11 08:33:34| CRI


 

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS) umepongeza hatua ya Sudan Kusini ya kuongeza muda wa serikali ya mpito.

Katika taarifa yake, UNMISS imesema hatua hiyo itawezesha utekelezaji wa majukumu muhimu ambayo hayajakamilika katika makubaliano ya amani. Pia umezitaka pande zote zilizosaini makubaliano hayo kufanya kazi kwa pamoja, na kutekeleza kikamilifu majukumu muhimu yaliyobaki ili kuhakikisha kuwa, mazingira mazuri yanaanzishwa kwa ajili ya uchaguzi huru, na wa haki na kuaminika mwishoni mwa muda ulioongezwa.

Wiki iliyopita, vyama mbalimbali vya Sudan Kusini vilikubaliana kuongeza muda wa serikali ya mpito kwa miezi 24.