Mashirika ya kibinadamu yatafuta ulinzi bora kwa raia mashariki mwa DRC
2022-08-12 08:47:00| cri

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric amesema, wafanyakazi wa mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wametoa wito wa ulinzi bora kwa raia nchini humo.

Bw. Dujarric alisema,  mapema mwezi uliopita, makundi yenye silaha yamewaua raia 100, kuteka nyara zaidi ya watu 93, wakiwemo watoto, na kusababisha zaidi ya watu 96,000 kupoteza makazi yao.

Amesema watu hao hawana uwezo wa kulima mashamba yao, ambayo ni chanzo kikuu cha kipato kwa raia wengi,  akiongeza kuwa, mahitaji ya dharura kwa watu walioathiriwa na mashambulizi hayo ni ulinzi, chakula, malazi, na bidhaa zisizo za chakula pamoja na huduma za matibabu.