Askari 42 wauawa katika shambulizi la kigaidi nchini Mali
2022-08-12 09:03:38| CRI


 Askari 42 wa jeshi la Mali waliuawa na wengine 22 kujeruhiwa katika shambulizi la kigaidi lililotokea karibu na mji wa Tessit, mkoa wa Gao nchini humo.

Taarifa iliyotolewa na serikali ya nchi hiyo inasema magaidi hao ambao wanashukiwa kutokea Kundi la ISGS, walitumia droni , mizinga na mabomu, na takriban magaidi 39 pia wameuawa katika shambulizi hilo katika eneo la mpaka wa Mali, Niger na Burkina Faso.

Mali imekuwa ikikabiliwa na migogoro ya kiusalama, kisiasa na kiuchumi tangu mwaka 2012, na uasi, ugaidi na ghasia za kijamii zimesababisha vifo vya maelfu ya watu na kuwafanya malaki ya wengine kukimbia makazi yao.