Tanzania kujenga barabara zenye urefu wa zaidi ya kilomita elfu 33 mwaka wa fedha 2022/2023
2022-08-15 09:23:05| CRI

Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini wa Tanzania (TARURA) imesaini mikataba 10 na kampuni za ndani kwa niaba ya wakandarasi 969 inayohusu ujenzi wa barabara zenye urefu wa zaidi ya kilomita 33,091 nchini humo katika mwaka wa fedha 2022/2023.

Mikataba hiyo ilisainiwa mjini Dodoma ikishuhudiwa na rais Samia Suluhu Hassan. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Innocent Bashungwa amesema miradi husika inayotarajiwa kugharimu shilingi bilioni 331.39 za Tanzania itatelekezwa katika mwaka huu wa fedha, ikiwemo ujenzi wa madaraja 269. Kati ya barabara hizo, barabara zenye urefu wa kilomita 21,593 zimepangwa kukarabatiwa.

Rais Samia amesema ujenzi na ukarabati wa barabara utasaidia ustawi wa maisha ya Watanzania walioko vijijini, na ameagiza TARURA kusimamia vizuri ujenzi husika ili kuhakikisha ubora wake unafikia viwango vinavyohitajika.