Ethiopia yafungua mradi mkubwa wa barabara uliojengwa na China mjini Addis Ababa
2022-08-16 08:36:54| CRI

Ethiopia imezindua mradi mkubwa wa barabara ya makutano yenye urefu wa kilomita 3.8, ukiunganisha vipande vitatu vya barabara na ujenzi wa handaki la njia mbili lenye urefu wa mita 320.

Meya wa mji wa Addis Ababa Bibi Adanech Abiebie amesema kwenye ufunguzi kuwa mradi huo unaonesha nia thabiti ya Ethiopia, ya kuendeleza miradi muhimu ya maendeleo katika kipindi kifupi na kwa ubora wa hali ya juu. Ameishukuru serikali ya China na watu wake kwa kugharamia na kutekeleza mradi huo.

Ofisa mkuu mwandamizi wa ubalozi wa China nchini Ethiopia Bw. Shen Qinmin amesema mradi huo ni alama ya ushirikiano na urafiki kati ya China na Ethiopia. Amesema pande hizo mbili zinafuata mikakati ya maendeleo ambayo inaendana, na zina ushirikiano wa kunufaishana ambao unatoa mwelekeo wa jumla wa ushirikiano kati ya China na Afrika.