Polisi Tanzania waharibu hekta 75 za bangi ndani ya miezi saba
2022-08-17 08:30:19| CRI

Polisi nchini Tanzania wametangaza kuwa wameharibu hekta 75 za bangi katika mkoa wa Kaskazini wa Mara.

Kamanda wa polisi eneo maalumu la Tarime/Rorya, Bw. Geoffrey Sarakikya, amesema polisi wamekamata jumla ya kilo 4,298 za bangi kwenye operesheni maalumu iliyoanza Januari hadi Julai dhidi ya mashamba ya bangi katika wilaya sita za mkoa wa Mara.

Kwa mujibu wa ofisa huyo, jumla ya washukiwa 110 wamekamatwa kwenye operesheni hiyo kwa tuhuma za kulima na kusafirisha bangi.