Kiongozi wa upinzani wa Kenya asema atapinga matokeo ya urais mahakamani
2022-08-17 08:28:10| CRI

Kiongozi wa upinzani wa Kenya Bw. Raila Odinga amekataa matokeo ya uchaguzi wa rais yaliyotangazwa na tume huru ya uchaguzi na uratibu wa mipaka ya Kenya yaliyompatia ushindi Bw. William Ruto. Bw. Odinga amesema tume ya uchaguzi imekiuka katiba na kushindwa kufikia moyo wa maridhiano.