Kenya yahimiza kurejeshwa kwa shughuli za kawaida za biashara baada ya uchaguzi
2022-08-17 08:29:02| CRI

Mamlaka za usalama nchini Kenya zimewataka raia na wafanyabiashara kurejesha shughuli zao za kawaida kufuatia kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.

Mkuu wa Huduma za Umma na Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri wa Usalama wa Taifa (NSAC) Bw. Joseph Kinyua, ametoa wito huo kupitia taarifa iliyotolewa mjini Nairobi.

Taarifa hiyo imekuja kufuatia Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kumtangaza Bw. Willam Ruto kuwa rais mteule wa awamu ya tano, baada ya kupata asilimia 50.49 ya kura kwenye uchaguzi mkuu.