Rais Xi asisitiza ustawishwaji wa sehemu ya kaskazini mashariki mwa China
2022-08-19 08:45:59| CRI

Rais Xi Jinping wa China amesisitiza hisia kubwa za uwajibikaji na juhudi kwenye ustawishwaji mpya wa sehemu ya kaskazini mashariki mwa China katika zama mpya.

Katika ziara yake ya ukaguzi mkoani Liaoning kuanzia Jumanne hadi Jumatano wiki hii, Rais Xi ametoa wito wa kupanua wigo wa ustawishwaji na maendeleo ya mkoa huo.

Amesema juhudi zaidi zinatakiwa ili kuhimiza maslahi ya pamoja kwa wote, kusukuma mbele juhudi za kuufanya mfumo na uwezo wa utawala wa China uwe wa kisasa, na kuimarisha utawala kamili na wa kina wa Chama, ili kuweka msingi kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China.