Waziri wa mambo ya nje wa China atoa mapendekezo ya kujenga jumuiya ya China na Afrika yenye mustakbali wa pamoja
2022-08-19 08:27:47| CRI

Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi ametoa pendekezo la kujenga jumuiya ya China na Afrika yenye mustakbali wa pamoja katika zama mpya, kwenye mkutano kuhusu mapitio ya maendeleo yaliyopatikana kupitia ushirikiano kati ya China na Afrika.

Kwenye mkutano huo uliofanyika kwa njia ya video kuhusu utekelezaji wa mambo yaliyokubaliwa kwenye mkutano wa 8 wa mawaziri wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), Bw. Wang amesema China na Afrika zimetekeleza kwa pamoja makubaliano yaliyofikiwa kwa maendeleo mazuri na kuwa na matokeo yanayoonekana kwa watu wa Afrika.

Akikumbusha kuwa mwaka huu Umoja wa Afrika unaadhimisha miaka 20 tangu kuanzishwa kwake, Bw. Wang amesema China na Afrika zinatakiwa kushirikiana zaidi kutafuta maendeleo ya pamoja, na kujenga jumuiya ya China na Afrika yenye mustakbali wa pamoja katika zama mpya.