UM walaani mashambulizi dhidi ya wafanyakazi wa misaada nchini Sudan Kusini
2022-08-19 08:46:38| CRI

Shirika la misaada ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa limelaani mashambulizi dhidi ya wafanyakazi wa misaada nchini Sudan Kusini, likisema matukio kama hayo yanaweza kuathari vibaya usambazaji wa msaada wa chakula kwa watu wenye mahitaji.

Mratibu wa misaada ya kibinadamu nchini Sudan Kusini Bibi Sara Beysolow Nyanti,, pia ametoa wito wa hatua za pamoja kuchukuliwa ili kutatua msukosuko wa kibinadamu na kutokomeza mara moja mashambulizi dhidi ya raia na wafanyakazi wa kibinadamu.

Kwa mujibu wa ofisa huyo, watu milioni 8.9 nchini Sudan Kusini wanahitaji msaada wa kibinadamu mwaka huu, na mashirika ya misaada yanawalenga watu milioni 6.8 walioathiriwa na mabadiliko ya tabianchi, ukame, machafuko, janga la Uviko-19 na mengineyo.