Majimbo sita ya Sudan yaingia katika hali ya tahadhari kutokana na mvua kubwa na mafuriko
2022-08-22 10:28:44| CRI

Shirika la habari la Sudan SUNA liliripoti kuwa serikali ya Sudan Jumapili ilitangaza kuwa majimbo sita yameingia katika hali ya dharura na tahadhari kutokana na mvua kubwa na mafuriko.

Ripoti imesema katika mkutano wa Jumapili, baraza la mawaziri lilitangaza majimbo sita yanayokumbwa na mvua kubwa na mafuriko yanaingia katika hali ya dharura na tahadhari, yakiwemo River Nile, Gezira, White Nile, West Kordofan, Darfur Kusini na Kassala. Baraza hilo lilisisitiza kuwa msaada wa kibinadamu wa ndani na nje kutoka serikali na jamii unahitajika, ili kuwasaidia watu wanaoathiriwa katika majimbo hayo.