Idadi ya vifo kutokana na mvua kubwa na mafuriko nchini Sudan yafikia 83
2022-08-23 09:44:59| CRI

Baraza la Ulinzi wa Raia la Kitaifa la Sudan limesema kuwa idadi ya watu waliofariki kutokana na mvua kubwa iliyonyesha hivi karibuni na kufuatiwa na mafuriko nchini Sudan imepanda hadi 83.

Wakati huo huo, zaidi ya nyumba 18,000 ziliteketea na nyingine 25,000 kuharibiwa katika maeneo yaliyoathiriwa.

Taarifa imesema kuwa Wizara ya umwagiliaji na rasilimali za maji ilionya kwamba viwango vya maji katika mito ya Blue Nile na White Nile vinatarajiwa kuongezeka tena katika siku mbili zijazo. Wizara hiyo iliwataka watu wanaoishi karibu na mito hiyo miwili, hasa katika mji mkuu Khartoum, kuchukua tahadhari zinazohitajika.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, kuanzia mwezi Juni takriban watu 136,000 wameathiriwa na mafuriko na mvua kubwa nchini kote.