Watu wasiopungua laki tisa wakabiliwa na hatari ya uhaba wa chakula kaskazini mwa Msumbiji
2022-08-23 09:48:37| CRI

Mamlaka za usalama wa chakula nchini Msumbiji jana zilionya kuwa watu wasiopungua laki tisa wanaweza kukabiliwa na uhaba wa chakula huko mkoani Cabo Delgado, kaskazini mwa nchi hiyo.

Akiongea na wanahabari wakati wa mkutano wa 11 wa Baraza la Ushauri la Sekretarieti ya Kiufundi juu ya Usalama wa Chakula na Lishe uliofanyika mjini Maputo, katibu mtendaji Bibi Leonor Mondlane alisema, taasisi yake inafuatilia kwa makini hali ya uhaba wa chakula.

Alisema mapambano huko Cabo Delgado yamewalazimisha watu waache mashamba yao, na mvua zisizo za kawaida pamoja na sababu nyingine zimepeleka uhaba wa chakula. Aliongeza kuwa hali hiyo itarekebishwa katika siku zijazo kutokana na hatua zinazochukuliwa kwenye sehemu mbalimbali za nchi hiyo.