UM kuisaidia Afrika kuendeleza masoko ya mitaji ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi
2022-08-24 09:31:01| CRI

Umoja wa Mataifa jana ulisema utazisaidia nchi za Afrika kuendeleza masoko ya mitaji ili kuharakisha maendeleo ya kiuchumi.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Fedha na Masoko ya Mitaji pamoja na Kitengo cha Maendeleo ya Sekta Binafsi na Fedha katika Kamisheni ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa barani Afrika (UNECA) Bibi Sonia Essobmadje alisema, masoko ya mitaji barani Afrika hayajaendelezwa na kupelekea fedha zilizopo kuwa na ukomo kwa mashirika binafsi na miradi ya umma.

Ameongeza kuwa masoko ya mitaji ambayo yameendelezwa vizuri yatatoa fursa kwa mitaji ya nje inayotafuta nafasi za uwekezaji barani Afrika. Masoko hai ya mitaji ya ndani yatapunguza utegemezi wa Afrika kukopa nchi za nje ili kufadhili miradi ya maendeleo.