Reli ya Ethiopia-Djibout yaanza kusafirisha magari
2022-08-26 09:50:10| CRI

Reli ya Ethiopia-Djibout iliyojengwa na China imeanza kusafirisha magari kutoka bandari ya Djibouti hadi Addis Ababa.

Shehena ya kwanza ya magari ilifikishwa katika kituo cha mizigo cha Indobe kwenye viunga vya Addis Ababa, ambapo hafla fupi ilifanywa ili kupokea shehena hiyo ya kwanza.

Afisa Mtendaji mkuu wa Kampuni ya Reli ya Pamoja kati ya Ethiopia na Djibout Abdi Zenebe amepongeza hatua hiyo, akisisitiza kuwa itasaidia kutimiza matarajio makubwa ya reli kwa upande wa kuwezesha mfumo wa usafirishaji wa Ethiopia.

Reli hiyo ambayo imejengwa na Kampuni ya Uhandisi wa Reli ya China (CREC) na Kampuni ya Uhandisi na Ujenzi (CCECC) za China, ni reli ya kwanza ya kasi ya kuvuka mpaka katika bara la Afrika.