Odinga aahidi kusuluhisha mgogoro wa uchaguzi kwa amani nchini Kenya
2022-08-29 09:13:31| CRI

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga amemuahidi katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kuwa mgogoro wa uchaguzi nchini humo utasuluhishwa kwa njia ya amani.

Odinga amewasilisha pingamizi mahakamani, akipinga matokeo ya uchaguzi wa urais yaliyotangazwa na tume ya uchaguzi tarehe 15 Agosti, ambapo mshindani wake mkuu William Ruto, ambaye alikuwa naibu rais wa sasa wa nchi hiyo alitangazwa kuwa mshindi, na kusema ataheshimu uamuzi wa mahakama kuu. 

Kwenye mazungumzo hayo, Guterres alimpongeza Odinga kwa kuamua kutoa pingamizi lake la matokeo ya uchaguzi wa urais kupitia taasisi za kidemokrasia na kisheria na mahakama kuu.

Naye Odinga alimshukuru Guterres kwa kuzungumza naye akisema, hatua hiyo imeonesha heshima yake kwa taifa la Kenya na umuhimu wa utulivu wa nchi hiyo kwa dunia.