Watu 23 wauawa katika vurugu mjini Tripoli, Libya
2022-08-29 09:27:26| CRI


 

Wizara ya Afya ya Libya imesema, watu 23 wameuawa na wengine 140 kujeruhiwa kwenye mapambano yaliyotokea katika mji mkuu wa nchi hiyo Tripoli.

Vyombo vya habari nchini Libya vimesema, vikosi vya jeshi la Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya na bunge la nchi hiyo vilipambana katika sehemu kadhaa mjini Tripoli.

Taarifa zilizotolewa na Wizara ya Afya ya nchi hiyo zimesema, baadhi ya hospitali na vituo vya afya pia vilishambuliwa katika mapambano hayo.