Rais wa Tanzania aahidi kumaliza ukosefu wa usawa wa kijinsia katika uteuzi wa majaji
2022-08-30 08:36:55| CRI

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameahidi kumaliza ukosefu wa usawa katika uteuzi wa majaji ili kuimarisha utekelezaji wa haki katika nchi hiyo.

Akizungumza baada ya kuwaapisha majaji wapya 21 wa mahakama ya juu na mahakama ya rufani aliowateua hivi karibuni, rais Samia amesema uwiano wa majaji wanawake na wanaume kwa sasa ni 50/37, na utafikia 50/50 hivi karibuni.

Amesema uzoefu umeonesha kuwa, mahakimu wanawake wanawazidi wenzao wa kiume katika utendaji kazi kwa msingi wa masuala ya uadilifu, na kuongeza kuwa, kuongezeka kwa majaji wanawake, pamoja na kudumisha taaluma, kumeimarisha utendaji kazi katika mahakama.