Kundi la NCBA la Kenya kushirikiana na Huawei kuzindua huduma za kifedha za kidijitali
2022-08-30 08:35:47| CRI

Taasisi ya huduma za kifedha nchini Kenya NCBA imesema kuwa itashirikiana na kampuni ya mawasiliano ya China Huawei ili kuanzisha bidhaa za kibenki za kidijitali kwa wateja wake.

Mkurugenzi mtendaji wa NCBA John Gachora amewaambia wanahabari jijini Nairobi kuwa, kampuni ya Huawei ina uwezo wa kuendeleza programu tumizi za kidijitali katika simu zinazowezesha malipo ya kifedha kufanyika kati ya sarafu ya nchi husika na sarafu kubwa za kigeni.

Amesema Kundi la NCBA litaongeza kasi ya kuingia kwenye huduma za kifedha za kidijitali kwa kuwa zitawezesha wakopeshaji kuimarisha ufanisi wa operesheni zao kwa kuruhusu wateja kupata huduma za kifedha mahali na muda wowote.