Ushirikiano kati ya Afrika na China wapata mafanikio mazuri
2022-08-30 08:39:50| CRI

Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa China kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam nchini Tanzania, Profesa Humphrey Moshi amesema ushirikiano kati ya Afrika na China umepata mafanikio mazuri, na umeleta faida halisi kwa watu wa Afrika.

Profesa Moshi amesema hayo alipohojiwa na Shirika la Habari la China Xinhua. Amesema katika miaka ya hivi karibuni, ushirikiano kati ya pande hizo mbili umetoa mchango mkubwa katika kupunguza umaskini, kuboresha mazingira ya uwekezaji, kuinua kiwango cha viwanda na kuhimiza maendeleo ya uchumi kwa nchi za Afrika.

Pia amesisitiza kuwa, China inatetea utaratibu wa pande nyingi, na kujikita katika kuhimiza ushirikiano wa kimataifa wa kupambana na janga la virusi vya Corona, ikiwa ni pamoja na kutoa vifaa vya matibabu na chanjo za COVID-19 kwa nchi nyingi barani Afrika, na kufanya ushirikiano ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kupunguza umaskini. Katika miaka ya hivi karibuni, ushirikiano kati ya Afrika na China pia umepata maendeleo kwa udhahiri katika kukabiliana na COVID-19 na kufufua ukuaji wa uchumi.