China yapongezwa kwa mafanikio katika maendeleo
2022-08-30 10:08:29| CRI


 

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Urafiki kati ya Sudan Kusini na China Balozi Emmanuel LoWilla amesema China imepata mafanikio makubwa ya kushangaza katika machakato wa maendeleo.

Akizungumzia maoni yake juu ya uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Balozi LoWilla amesema chini ya Chama hicho chenye historia ya zaidi ya miaka 100, China, ikiwa nchi inayoendelea, imepata mafanikio ya kushangaza, na sasa inashika nafasi ya pili duniani kwa ukubwa wa uchumi.

Kuhusu uhusiano kati ya Sudan Kusini na China, Balozi LoWilla amesema nchi hizo mbili zinadumisha uhusiano wa karibu, na tangu kuanzishwa kwa nchi ya Sudan Kusini, China imetoa msaada mkubwa haswa uwekezaji muhimu kwa nchi hiyo changa, na hivi sasa kuna Wachina wengi wanaoishi na kufanya kazi nchini Sudan Kusini.