Chama tawala cha Angola chashinda uchaguzi mkuu
2022-08-31 09:19:07| CRI

Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Angola (CNE) imetangaza kuwa, Chama tawala nchini humo Harakati za Wananchi za Ukombozi wa Angola (MPLA) kimeshinda uchaguzi mkuu uliofanyika wiki iliyopita, kwa kupata asilimia 51.17 ya kura.

CNE imesema Chama cha UNITA ambacho ni chama kikuu cha upinzani nchini humo, kimepata asilimia 43.95 ya kura. Matokeo ya mwisho yameonyesha kuwa, chama cha MPLA kimepata viti 124 kati ya 220 vya Bunge, na UNITA imeshika nafasi ya pili bungeni kwa kupata viti 90.

Kwa mujibu wa katiba ya Angola, mgombea mkuu wa chama cha siasa ambacho kitapata kura nyingi kwenye uchaguzi, atakuwa rais kwa mihula isiyozidi miwili.